25. Shetani Anamjaribu Yesu

25. Shetani Anamjaribu Yesu — picha 1

Mara tu Yesu alipokwisha kubatizwa, Roho Mtakatifu alimwongoza Yesu nyikani, huko alifunga siku arobaini mchana na usiku. kisha Shetani alifika kumjaribu Yesu ili atende dhambi.

25. Shetani Anamjaribu Yesu — picha 2

Shetani alimjaribu Yesu akisema; "Kama wewe ni mwana wa Mungu yaamuru mawe haya yawe mikate upate kula".

25. Shetani Anamjaribu Yesu — picha 3

Yesu akajibu; "Imeandikwa katika neno la Mungu, watu hawahitaji mkate pekee ili wapate kuishi, bali wanahitaji kila neno linalosemwa na Mungu".

25. Shetani Anamjaribu Yesu — picha 4

Kisha Shetani alimchukua Yesu mpaka juu ya mnara wa hekalu na kumwambia; "Kama wewe ni Mwana wa Mungu jirushe mwenyewe chini, kwa vile imeandikwa, Mungu atakuagizia malaika wake wakuchukue ili usijigonge mguu wako katika jiwe".

25. Shetani Anamjaribu Yesu — picha 5

Lakini Yesu alimjibu Shetani kwa kunukuu Maandiko akisema; " Katika neno la Mungu, anaagiza watu wake, usimjaribu Bwana Mungu wako".

25. Shetani Anamjaribu Yesu — picha 6

Kisha Shetani alimwonyesha Yesu falme zote za ulimwengu na fahari zake zote na akasema; "Nitakupa hivi vyote iwapo utanisujudia na kuniabudu mimi".

25. Shetani Anamjaribu Yesu — picha 7

Yesu akajibu; ondoka kwangu Shetani! Katika neno la Mungu ameagiza, "Mwabudu Bwana Mungu wako na kumtumikia Yeye peke yake".

25. Shetani Anamjaribu Yesu — picha 8

Yesu hakujitia chini ya majaribu ya Shetani, hivyo Shetani aliondoka akamwacha. kisha malaika walikuja na kumhudumia Yesu.

_Simulizi ya Biblia Kutoka: Mathayo 4:1-11;_

Marko 1:12-13; Luka 4:1-13

Soma katika kisomaji

Bila malipo kutumia, kubadilisha na kushiriki chini ya leseni huria (CC BY-SA 4.0).