34. Yesu Anafundisha Mambo Mengine

34. Yesu Anafundisha Mambo Mengine — picha 1

Yesu aliwaambia masilimuzi mengi kuhusu ufalme wa Mungu .Kwa mfano,alisema,"Ufalme wa Mungu ni kama punje ya haradali ambayo mtu aliipanda shambani mwake.Unajua kwamba punje ya haradali ni ndogo kuliko punje zote."

34. Yesu Anafundisha Mambo Mengine — picha 2

"Lakini wakati punje ya haradali inapokuwa, inakuwa kubwa kuliko mimea yote bustanini, inakuwa na ukubwa wa kutosha hata ndege huja na kutua kwenye matawi yake,"

34. Yesu Anafundisha Mambo Mengine — picha 3

Yesu akawaambia simulizi nyingine ,"Ufalme wa Mungu ni kama amira aliyoichanganya mwanamke kwenye baadhi ya donge la mkate na mpaka kusambaa kwenye donge lote."

34. Yesu Anafundisha Mambo Mengine — picha 4

"Ufalme wa Mungu pia unafanana kama hazina ambayo mtu ameificha shambani.Mtu mwingine akaikuta hazina hiyo na kuifukia tena. Alijawa na furaha kiasi kwamba akaenda kuuza kila kitu alichonacho na akatumia fedha hiyo kununua shamba hilo."

34. Yesu Anafundisha Mambo Mengine — picha 5

"Ufalme wa Mungu pia ni kama lulu kamili ya thamani kubwa .Mfanyabiashara wa lulu alipoipata, aliuza vitu vyote alivyokuwanavyo na kutumia fedha hiyo kununua hiyo lulu.

34. Yesu Anafundisha Mambo Mengine — picha 6

Tena Yesu akawaambia simulizi ya baadhi ya watu ambao wameweka tumaini katika matendo yao mema na kudharau watu wengine .Akasema. "Watu wawili walikwenda hekaluni kusali .Mmoja alikuwa mtoza ushuru na mwingine kiongozi wa dini."

34. Yesu Anafundisha Mambo Mengine — picha 7

"Kiongozi wa dini aliomba hivi. 'Asante, Mungu kwamba mimi siyo mwenye dhambi kama watu wengine - mfano wanyanganyi, wasio haki, wazinzi, au hata kama huyu mtoza ushuru'".

34. Yesu Anafundisha Mambo Mengine — picha 8

"Kwa mfano, nafunga mara mbili kwa wiki na kukutolea moja ya kumi ya pesa zote na mali zote nizipatazo."

34. Yesu Anafundisha Mambo Mengine — picha 9

"Lakini mtoza ushuru alisimama mbali na kiongozi wa dini hata hakuelekeza uso wake mbinguni. Badala yake alijipiga ngumi kifua chake na akaomba, "Mungu, tafadhali unirehemu mimi kwa sababu ni mwenye dhambi."

34. Yesu Anafundisha Mambo Mengine — picha 10

"Kisha Yesu akasema, "Lakini nawaambieni ukweli, Mungu alisikia maombi ya mtoza ushuru na kumtangaza kuwa mwenye haki. Lakini hakuyapenda maombi ya kiongozi wa dini. Mungu humshusha kila ajikwezae na humpandisha kila ajinyenyekezaye,"

Simuliziya Biblia kutoka: Mathayo 13:31-33; 44-46; Marko 4:30-32,; Luka 13:18-21; 18:9-14

Soma katika kisomaji

Bila malipo kutumia, kubadilisha na kushiriki chini ya leseni huria (CC BY-SA 4.0).