37. Yesu Amfufua Lazaro kutoka Wafu

37. Yesu Amfufua Lazaro kutoka Wafu — picha 1

Siku moja, Yesu alipata habari kuwa Lazaro ni mgonjwa sana. Lazaro na dada zake wawili- Martha na Maria walikuwa marafiki wa karibu wa Yesu. Yesu alipopata habari hizi alisema, "Huu si ugonjwa wa kifo, bali ni ugonjwa wa kumtukuza Mungu." Yesu aliwapenda marafiki zake, lakini alisubiri hadi siku mbili.

37. Yesu Amfufua Lazaro kutoka Wafu — picha 2

Baada ya siku mbili, Yesu aliwaambia wanafunzi wake, ''Twendeni tena Uyahudi." "Lakini mwalimu. " Wanafunzi wake walisema, "Muda mfupi tu uliopita watu walitaka kukuua!" Yesu alisema "Rafiki yetu Lazaro amelala usingizi na ni lazima nimwamshe."

37. Yesu Amfufua Lazaro kutoka Wafu — picha 3

Wanafunzi wa Yesu walijibu, "Bwana, kama Lazaro amelala, basi atapata nafuu." Yesu aliwaambia wazi, "Lazaro amekufa, nafurahi kuwa sikuwepo ili mpate kuniamini."

37. Yesu Amfufua Lazaro kutoka Wafu — picha 4

Yesu alipofika katika mji wa Lazaro, Lazaro alikuwa tayari amekufa kwa siku nne. Martha alikwenda kumwona Yesu akasema, "Bwana, kama ungekuwa hapa, kaka yangu asingekufa . Lakini ninaamini kuwa Mungu atakupa chochote umwombacho."

37. Yesu Amfufua Lazaro kutoka Wafu — picha 5

Yesu akajibu akasema, "Mimi ni Ufufuo na Uzima, yeyote aniaminiye ataishi, hata kama akifa. Kila aniaminiye hatakufa. Unaamini hivyo?" Martha akajibu, "Ndiyo Bwana ninaamini kuwa wewe ni Masihi, Mwanawa Mungu."

37. Yesu Amfufua Lazaro kutoka Wafu — picha 6

Maria alipofika. Alianguka miguuni pa Yesu akasema, "Bwana, kama wewe tu ungekuwepo kaka yangu asingekufa." Yesu akawauliza, "Mmemuweka wapi Lazaro?" Walimjibu " Kaburini, njoo uone." Yesu alilia.

37. Yesu Amfufua Lazaro kutoka Wafu — picha 7

Kaburi lilikuwa pango limefunikwa na jiwe. Yesu alipofika kaburini aliwaambia, "Liondoeni jiwe." Lakini Martha alisema, "Amekuwa kaburini sasa siku nne, ananuka!"

37. Yesu Amfufua Lazaro kutoka Wafu — picha 8

Yesu alijibu, "Je, sikusema kuwa kama ukiniamini utaona utukufu wa Mungu?" Ndipo wakaliondoa jiwe.

37. Yesu Amfufua Lazaro kutoka Wafu — picha 9

Basi Yesu alitazama juu mbinguni akasema, "Baba, asante kwa kuwa unanisikia. Tena najua wewe hunisikia siku zote. Lakini nimesema haya kwa ajili ya watu hawa waliosimama hapa, kwa kuwa wataamini kuwa ulinituma." Kisha Yesu akapaza sauti, "Lazaro, njoo nje."

37. Yesu Amfufua Lazaro kutoka Wafu — picha 10

Ndipo Lazaro alitoka nje! Alikuwa bado amefungwa sanda, Yesu akawaambia, "Msaidieni kuondoa sanda na mwacheni huru!." Wayahudi wengi walimwamini Yesu kwa sababu ya muujiza huu.

37. Yesu Amfufua Lazaro kutoka Wafu — picha 11

Lakini viongozi wa dini ya kiyahudi waliona wivu, ndipo wakakusanyika pamoja kupanga watakavyoweza kumuua Yesu na Lazaro.

Simulizi ya Biblia kutoka: Yohana 11:1-46

Soma katika kisomaji

Bila malipo kutumia, kubadilisha na kushiriki chini ya leseni huria (CC BY-SA 4.0).