39. Yesu Anashitakiwa.

39. Yesu Anashitakiwa. — picha 1

Ilikuwa usiku wa manane wakati huo. Askari wakampeleka kwenye nyumba ya kuhani mkuu ili kumhoji. Petro akawafuata kwa mbali nyuma yao. Wakati Yesu anachukuliwa kwenye nyumba, Petro alikuwa nje peke yake akiota moto.

39. Yesu Anashitakiwa. — picha 2

Ndani ya Nyumba viongozi wa kiyahudi wakamshitaki Yesu. Wakaleta mashahidi wengi wa uongo walioshuhudia uongo dhidi ya Yake. vile vile hata maelezo yao yalitofautiana kila mmoja alisema tofauti. kwa hiyo viongozi wa kiyahudi hawakukubaliana kama alikuwa na hatia yeyote. Yesu hakusema chochote.

39. Yesu Anashitakiwa. — picha 3

Hatimaye kuhani mkuu akamwangalia Yesu na kusema "Tuambie wewe ni Masihi mwana wa Mungu aliye hai?"

39. Yesu Anashitakiwa. — picha 4

Yesu akamjibu, "Mimi ndiye, utaniona nimekaa na Mungu na pia nikishuka kutoka mbinguni" Kuhani mkuu akararua mavazi yake kwa hasira na akasema kwa sauti kuu kwa viongozi wa kidini wengine "Hatuhitaji mashahidi zaidi ya hawa! Mmesikia toka kwake mwenyewe, akisema yeye ni mwana wa Mungu. Hukumu yenu ni ipi?"

39. Yesu Anashitakiwa. — picha 5

Viongozi wa kiyahudi wote wakamjibu kuhani mkuu kuwa "Anastahili kufa" baadaye wakamfunika macho Yesu, wakamtemea mate, wakampiga, na kumdhihaki.

39. Yesu Anashitakiwa. — picha 6

Na Petro alikuwa inje ya nyumba akisubiri. Mtumishi mmoja msichana akamwona na akamwambia "Na wewe pia ulikuwa na Yesu!" Petro akakana. baadaye binti mwingine akasema kitu hichohicho. Na petro akakataa tena. hatimaye watu wakasema "Tunajua wewe ulikuwa pamoja naye maana ninyi nyote ni wenyeji wa Galilaya.

39. Yesu Anashitakiwa. — picha 7

tena Petro akaapa, akisema, "Mungu wangu na anilaani kama mimi namjua mtu huyu!" Mara ghafla Jogoo akawika na Yesu akageuka kumwangalia Petro.

39. Yesu Anashitakiwa. — picha 8

Petro akaondoka na akilia kwa huzuni kubwa. Wakati huo huo, Yuda, mwenye kumsaliti Yesu, akaona kwamba viongozi wa kiyahudi wamemweka Yesu hatiani. Yuda akapatwa na huzuni kubwa sana na akaondoka mahali pale akaenda kujiua mwenyewe.

39. Yesu Anashitakiwa. — picha 9

Asubuhi na mapema, viongozi wa kiyahudi wakamleta Yesu kwa Pilato liwali wa Kirumi. wakitumaini kuwa Pilato atamhukumu Yesu kama mtu mwenye hatia na wakamwambia auawe. Pilato akamuuliza Yesu "Wewe ni mfalme wa wayahudi?"

39. Yesu Anashitakiwa. — picha 10

Yesu akamjibu "Wewe ndiye umesema hivyo, lakini ufalme wangu si ufalme wa dunia hii, kama ingekuwa hivyo watumishi wangu wangepigana kwa ajili yangu. Nimekuja ulimwenuni ili kuusema ukweli kuhusu Mungu. na kila mmoja anayependa huu ukweli hunisikiliza. Pilato akasema "Ukweli ni nini?"

39. Yesu Anashitakiwa. — picha 11

Baada ya kuongea na Yesu Pilato alitoka nje katika umati wa Watu na kusema "Nimeona hakuna hatia juu ya mtu huyu" lakini viongozi wa kiyahudi na makutano wote wakapiga kelele "Msulubishe" pilato akajibu "Hana hatia" lakini waliendelea kupiga kelele tena kwa nguvu. na Pilato akasema kwa mara ya tatu "Hana hatia yeyote"

39. Yesu Anashitakiwa. — picha 12

Pilato akaogopa kwamba makutano wataanza kuleta Ghasia, kwa hiyo aliwaruhusu askari wake kumsulubisha Yesu. Askari wa Kirumi wakampiga Yesu huku wakimpa vazi la kifalme na kofia iliyotengenezwa na miiba wakamvika. pia wakamdhihaki kwa kusema "Mtazame mfalme wa wayahudi"

Simulizi ya Biblia kutoka: Mathayo 26:57 - 27:26; Marko14:53-15:15; Luka 22:54-23:23; Yohana 18:12-19:16

Soma katika kisomaji

Bila malipo kutumia, kubadilisha na kushiriki chini ya leseni huria (CC BY-SA 4.0).